+255784519486 marampya@gmail.com

               Karibu Mara! Mbali na fursa za kijiografia, historia, hazina ya utamaduni na usalama; Mkoa wa Mara tunao utajiri wa rasilimali ardhi, maji, madini,  samaki mifugo na utalii.
Mara Mpya ni Mradi wa kukuza uchumi wa Mkoa wa Mara unaosimamiwa na Chemba ya Wafanyabiashara, Wakulima na Wenye viwanda wakishirikiana na Serikali ya Mkoa wa Mara. Mradi ulianzishwa mwezi Septemba 2019 ili kusaidia kuchochea uchumi na shughuli za kimaendeleo Mkoani Mara ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa maono ya MHE: SAMIA SULUHU HASSAN Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutaka sekta binafsi imsaidie namna ya kuwezesha taarifa na fursa muhimu za Serikali kuwafikia Wajasiriamali wadogo hasa vijijini na kuwasaidia kukuza uchumi wao.
Mkoa wa Mara ni chimbuko la viongozi mashuhuri nchini akiwemo Rais wa kwanza na Mhasisi wa Taifa hili Hayati Mwl.Julius K. Nyerere. Mkoa una fursa nyingi za kijiografia ukiwa unapakana na Nchi za Kenya na Uganda na kuufanya kuwa Lango muhimu  la Biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Huwezi kuongelea Utalii Barani Afrika bila kuitaja Hifadhi ya Serengeti, Hifadhi maarufu Sana duniani iliyo makazi ya the Big Five Twiga, Tembo, Simba, Chui na Nyati. Kwa sasa Mkoa wa Mara (Wilaya ya Bunda) ni Makao Makuu ya TANAPA(Tanzania National Parks) Kanda ya Magharibi inayohudumia Mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Geita, Kigoma na Kagera. Aidha Mkoa unazo fursa katika sekta za Kilimo, Uvuvi, Ufugaji, Madini n.k 
fahamu zaidi kuhusu Mkoa wa Mara

Fursa Zetu

Tangaza nasi

Hapari mpya

Tembelea habari mpya kutoka Marampya hili kujipatia Fursa Mbalimbali

0 ITEMS
0 /=