+255784519486 marampya@gmail.com
December 21, 2019 - BY Admin

MKUTANO WA WABUNIFU!

MKUTANO WA WABUNIFU!

Leo Marekani ni Taifa kubwa ktk nyanja kadhaa kwasababu ya nguvu ya Ubunifu, China sasa inatarajiwa kuipita Marekani kama Taifa kubwa Kiuchumi kwasababu ya nguvu ya Ubunifu.

Kila kitu unachokiona Duniani ni Wazo la mtu fulani ni Ubunifu wa mtu fulani uliobadilishwa kuwa kitu halisi. TCCIA tunaamini Kuna watu wana mawazo na Kuna watu Wabunifu ambao Mawazo yao na Ubunifu vikipewa nafasi vinaweza Kutatua changamoto ya ajira, maji Vijijini, changamoto za mitaji kwa Wajasiriamali, vinaweza ongeza ufaulu kwa wanafunzi, vinaweza saidia kampuni fulani kuongeza mauzo na faida, vinaweza kupunguza stress ktk maisha n.k. TCCIA MARA tunawaalika Watu Wabunifu Tukutane tuzungumze. Itakuwa tarehe 14/1/2021 Siku ya Alhamisi Saa 10. 30 Jioni Hotel ya LeGrande Mtaa wa Kennedy. Ni Mkutano huru hauna Kiingilio, Karibuni.


Tunahiji Kuibadili Taswira ya Mara na Tanzania

Boniface Ndengo Mkti wa TCCIA Mara Balozi wa Mara Mpya Trh 6/Jan/2021 Simu: 0784 519486

0 ITEMS
0 /=