+255784519486 marampya@gmail.com


Serikali inafanya jitihada kubwa sana kujenga miundombinu  ya barabara na mawasiliano. Mji wa Musoma ni moja ya miji iliyobuniwa kwa uzuri sana ambayo sasa barabara zake zote zimewekwa lami. Jitihada zinaendelea kujenga barabara za lami kufika maeneo mengi katika wilaya zingine na maeneo ya pembezoni kurahisha mawasiliano ndani ya Mkoa. Ziko barabara za Kimkakati zinazoendelea kujengwa kwa kiwango cha lami ikiwa ni pamoja na Musoma hadi Majita, Musoma hadi Arusha kupitia Serengeti, Barabara ya Kisorya hadi Nyamuswa kupitia Bunda, Barabara ya Tarime hadi Mugumu na Barabara ya Musoma hadi Mugumu zinaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami.

                  Miradi mingine katika eneo hili ni Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Julius Nyerere maarufu kama Kwangwa ni mradi wa zaidi ya Tshs 20 bilioni inatarajiwa kukamilika hivi karibuni. Tunayo miradi ya Maji, Miradi ya Umeme, hii yote inafungua fursa za uwekezaji na biashara ndani ya Mkoa.

0 ITEMS
0 /=